TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - (MDAs &LGAs)
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala wa Serikali na Mamlaka za Serikali za Mitaa (MDAs &LGAs) anapenda kuwataarifu waombaji kazi wote walioomba kazi kuwa usaili wa kuandika unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 14 - 15 Januari, 2023 katika kanda nne (4) za Dodoma, Mbeya, Mwanza na Dar es Salaam. Usaili utafanyika pia Zanzibar.
Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
i. Usaili utafanyika 14 hadi tarehe 15 Januari, 2023 kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili; muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada;
ii. Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa (Mask);
iii. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
iv. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia au Hati ya kusafiria;
v. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji;
vi. Wasailiwa watakaowasilisha“Testimonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hatiza matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI;
vii. Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi;
viii. Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili;
ix. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA);
x. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika;
xi. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi; na
xii. Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa siku ya usaili.
SOMA MATANGAZO HAYA RASMI KWA UKAMILIFU , KUPITIA LINK ZIFUATAZO :-